Masharti ya Huduma

Ilisasishwa mwisho: Desemba 2024

1. Uhusiano wa Kikataba

Masharti haya ya Matumizi ("Masharti") yanaongoza upatikanaji au matumizi yako ya programu, tovuti, maudhui, bidhaa, na huduma ("Huduma") zinazotolewa na Taksi Company Limited, kampuni binafsi ya dhima yenye mipaka iliyoanzishwa nchini Tanzania. TAFADHALI SOMA MASHARTI HAYA KWA MAKINI KABLA YA KUTUMIA HUDUMA. Matumizi yako ya Huduma yanamaanisha unakubaliana na Masharti haya, ambayo yanaunda uhusiano wa kikataba kati yako na Taksi Company Limited.

2. Huduma Zetu

Huduma hizi zinajumuisha mfumo wa teknolojia unaowawezesha watumiaji wa programu za Panda kupanga na kuratibu huduma za usafiri na wasambazaji wa huduma hizo. UNAKUBALI KUWA TAKSI COMPANY LIMITED HAITOI HUDUMA ZA USAFIRI BALI INAKUUNGANISHA NA WATOA HUDUMA BINAFSI AMBAO SI WAAJIRIWA WA TAKSI COMPANY LIMITED.

3. Matumizi Yako ya Huduma

Ili kutumia Huduma zetu, lazima ufungue akaunti ya mtumiaji. Lazima uwe na umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi. Usajili unahitaji kutoa taarifa zako kama jina, anwani, namba ya simu, umri, na njia moja ya malipo iliyohalalishwa.

4. Malipo

Unaelewa kuwa matumizi ya Huduma yanaweza kusababisha tozo kwako kwa huduma unazopokea. Taksi Company Limited itasimamia ukusanyaji wa malipo hayo kwa niaba ya mtoa huduma binafsi. Malipo yaliyofanywa kwa njia hii yatachukuliwa kama malipo uliyofanya moja kwa moja kwa mtoa huduma.

5. Kanusho; Ukomo wa Dhima; Fidia

TAKSI COMPANY LIMITED HAITAWAJIBIKA KWA HASARA ZA MOJA KWA MOJA AU ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA, IKIWEMO UPOTEVU WA FAIDA, DATA, MAJERAHA YA MWILI AU UHARIBIFU WA MALI UNAOTOKANA NA MATUMIZI YA HUDUMA HIZI.

6. Sheria Husika; Usuluhishi

Isipokuwa pale ilivyoelezwa vingine, Masharti haya yataongozwa na kufasiriwa kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro yoyote itatatuliwa kwanza kupitia usuluhishi kulingana na kanuni za Tiac (Tanzania International Arbitration Centre).

7. Wasiliana Nasi

Kwa maulizo yoyote ya kisheria au ufafanuzi, tafadhali wasiliana na idara yetu ya sheria kupitia Info@taksi.co.tz au tembelea ofisi zetu zilizopo Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.

Taksi Company Limited

P.O Box 13412, Ohio Street, Smart card House,
Dar es Salaam, Tanzania

Info@taksi.co.tz

By using Panda, you acknowledge that you have read and understood these terms.